Watu zaidi ya 17
wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa baada ya
mabasi waliokuwa wakisafiria kugongana katika kijiji cha Mlogolo
wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Ajali hiyo imetokea leo
majira ya saa 11 jioni baada ya Basi la Kampuni ya Sabena lenye namba
za usajiri T 110 ARV lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Mwanza kugongana
uso kwa uso na basi la AM Dreamline lenye namba za usajiri T 803 ATN
lililokuwa likitokea Mwanza kupitia Mpanda.

Pia inadaiwa kuwa dereva
wa basi la Sabena aliyefahamika kwa jina la James Kombe amepoteza
maisha baada ya kukatika kiwiliwili na kufa papohapo na kuwa jitihada za kutafuta kiwiliwili chake zilikuwa zikifanyika baada ya kupondeka vibaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi (Day-worker)

Mabasi yaliyohusisha
ajali hiyo ni basi la Sabena lililokuokea Mbeya kwenda -Mwanza na AM
Dreamline lililokuokea Mwanza kwenda Mpanda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni