Wake Up ..Filamu ya Kwanza Bongo
Kuchezwa na Mastaa Wengi
TASNIA ya filamu imezidi kukua na kusonga mbele kila siku,
thamani ya wasanii wanalipwa fedha nyingi kwa kushiriki filamu moja jambo
linalomfanya mtayarishaji kutumia wasanii wachache kwa filamu yake lake katika
sinema ya WAKE UP imevunja rekodi kuwashirikisha nyota wengi.
Akipiga stori kupitia
extra vaganza mtayarishaji wa
filamu hiyo Manaiki Sanga amesema kuwa sinema hiyo ilikuwa na kazi kubwa kwani
hata kama mwigizaji angetaka kuigiza bure shughuli ilikuwa kuwahudumia mahitaji
yao kwani ni mastaa wenye mahitaji makubwa katika maisha yao.
“Nashukru Mungu kwa kuniwezesha kufikia ndoto zangu kila siku
nilikuwa natamani kufanya kitu cha kipekee katika tasnia ya filamu na nimeweza
kuwashirikisha wasanii nyota wote ,”
“Nimetumia fedha nyingi sana
lakini lengo ni kuwa tofauti na wenzangu katika utayarishaji ilikuwa ni kazi
ngumu katika kuwapata na kuwashirikisha, namshukru sana Lamata Director wangu,”.
Filamu hiyo ambayo ipo tayari inatarajia kutoka mwezi wa nane
mwaka huu imewashirikisha wasanii kama Kajala Masanja, Amri Athuman ‘King
Majuto’, Hemed Suleiman, Irene Uwoya, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Tausi Mdegela,
Yusuf Mlela, Manaiki Sanga, Chuchu Hans, Mutrah, Asha Boko na nyota wanaofanya
vizuri katika filamu Bongo Movie.
Sinema hiyo ambayo inaleta mapinduzi katika tasnia ya filamu
Bongo itasambazwa na kampuni ya usambazaji wa filamu za kibongo ya Steps
Entertainment nchi nzima na kuona jinsi wasanii walivyoshindana humo na
kuinogesha filamu hiyo.