Alhamisi, 18 Juni 2015

Christian Bella ana ndoto za kufanya collabo na nani? Wema na Ubunge je? pia Rafiki wa Ben Pol kazungumzia walivyonusurika ajalini…#255 [Audio]


Kupitia  EXTRA  VAGANZA leo  tumebahatika kupiga  stori na mkali wa ‘Nani kama Mama’, Christian Bellaambaye ameelezea mastaa wa kimataifa ambao ana ndoto za kufanya nao Collabo kuwa ni Chriss Brown, Fally Ipupa, Wiz Kid pamoja na P Square.
EXTRA  VAGANZA imezungumza na Wema Sepetu ambaye  amethibitisha kuwa atagombea Ubunge viti maalum kupitia Mkoa wa Singida ambapo anatokea na sasa yupo Mkoani humo akihamasisha vijana kujiandikisha, anatarajia kuchukua fomu tarehe 15 mwezi ujao.

Kwa mujibu wake tayari ameanza kampeni ndogondogo za kuhakikisha anaingia mjengo..
Kingine kilichosikika  kwenye mtandao wa Instagram Ben Pol aliweka picha baada ya kunusurika kwenye ajali ya boti, rafiki yake wa karibu Fadhili alielezea na kusema walikua wakitoka kisiwa cha Mbudya na watu wengine, gafla mawimbi yakawa makubwa na hatimaye boti ikajaa maji, walikaa kwenye maji kwa zaidi ya saa moja, na baada ya kupiga kelel za msaada baadaye boti ya wavuvi ilikuja na kuwarushia kamba kuwakoa.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni