Ijumaa, 28 Novemba 2014

Bunge la Ufaransa kupiga kura kuitambua Palestina


Watunga sheria nchini Ufaransa hivi leo wanajadili hoja ya kuishinikiza serikali yao kulitambua dola la Palestina, kwa matarajio kwamba hatua hiyo itasaidia kuleta amani ya kudumu kwenye eneo la Mashariki ya Kati. Mjadala huo kwenye Bunge la Ufaransa unakuja huku kukiwa na uungwaji mkono wa hali ya juu barani Ulaya kwa ajili ya taifa la Palestina. Wengi wamevunjwa moyo na mkwamo kwenye mazungumzo ya amani, hatua za Israel kwenye Ukanda wa Gaza na utanuzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi. Inatarajiwa sana kwamba wabunge wa Ufaransa wataunga mkono hatua ya kuitaka serikali "kulitambua dola la Palestina kwa mtazamo wa kufikia makubaliano ya kudumu dhidi ya mzozo huo." Upigaji kura utakuwa wiki ijayo, ingawa bado rais wa nchi hiyo, Francois Hollande, atakuwa ndiye mwenye usemi wa mwisho. Hollande amesema anaunga mkono utambuzi wa kimataiga kwa taifa la Wapalestina na kwamba serikali yake inashinikiza kufufuliwa kwa mazungumzo ya amani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni