Shughuli za kuhesabu kura zaendelea Nigeria
Shughuli za kuhesabu kura zinaendelea nchini Nigeria katika uchaguzi wa rais na wabunge ambao ulifanyika siku ya Jumamosi na jana Jumapili. Kati ya vituo laki moja na nusu (150,000) vya kupigia kura, 300 viliendelea kufanya kazi jana, kufuatia hitilafu za kiufundi zilizovikumba Jumamosi.
Kwa kiasi kikubwa uchaguzi ulifanyika kwa amani, licha ya mashambulizi kadhaa katika eneo la kaskazini, ambayo kundi la Boko Haram limeshutumiwa kuyafanya. Watu wapatao milioni 60 walishiriki uchaguzi katika nchi hiyo yenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika.
Kiongozi wa zamani wa kijeshi wa Nigeria, Muhammadu Buhari, anatarajiwa kumpa changamoto kubwa rais wa sasa Goodluck Jonathan katika uchaguzi huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni