
Mpaka wa mataifa ya Maziwa Makuu kukiwemo DRC na Rwanda.
Wachunguzi kutoka jumuiya ya
mataifa ya eneo la maziwa makuu wamechapisha ripoti kuhusu mapigano ya
hivi karibuni yaliyotokea katika eneo la mpaka kati ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo na Rwanda.
Ripoti hiyo inasema kuwa mapigano hayo
yalitokana mzozo wa ardhi kati ya mataifa hayo mawili katika maeneo ya
milima miwili jirani. Mwandishi wetu wa Kinshasa Lubunga Byaombe
ameisoma ripoti hiyo na kutuandalia taarifa ifuatayo.Ripoti hiyo inasema kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa upande wake inasema kuwa Rwanda mara kwa mara haiheshimu mpaka ulio kati ya mataifa hayo mawili na wanajeshi wake huvuka mara kwa mara na kuingia katika taifa lake.
Hata hivyo ripoti hiyo inasema kuwa mapigano ya hivi majuzi yanatokana na kutokuwepo mpaka kamili kati ya mataifa hayo mawili.
Katika mapigano hayo ya hivi karibuni mataifa hayo yalikuwa yakizozania milima miwili ambayo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilidai yote ni yake huku Rwanda ikisema inamiliki mlima mmoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni