Syria yasema Muungano wa Marekani umeshindwa kuwaadhoofisha wanamgambo wa IS
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Syria Walid al-Moualem, amesema mashambulizi ya angani yanayoongozwa na Marekani yameshindwa kulidhoofisha kundi la wanamgambo wanaojiita Dola la Kiislamu nchini Syria. Walid al-Moualem ameongeza kuwa kundi hilo halitaweza kukabiliwa hadi pale Uturuki itakapolazimishwa kudhibiti mipaka yake huku akisema wanamgambo hao wanatumia mipaka hiyo kuingia nchini Syria. Aidha Muungano unaoongozwa na Marekani ulianza kuwashambulia wanamgambo wa dola la kiislamu katika ngome zao nchini Syria mwezi Septemba, kama mpango wa juhudi kubwa zaidi za kuliharibu kundi hilo lililodhibiti maeneo kadhaa nchini Syria na katika nchi jirani ya Iraq. Awali serikali ya Syria ilisema iko tayari kujiunga na mapambano dhidi ya wanamgambo wa IS lakini Marekani ikakataa kuwa na ushirikiano wa aina yoyote na rais Bashar al Assad inayosema amepoteza uhalali kwa kutekeleza mauaji ya raia wake na ni lazima aondokea madarakni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni