Watu zaidi ya 100 wauwawa katika shambulizi Nigeria
Mashambulizi ya mabomu na risasi yamelitikisa eneo la Kaskazini mwa Nigeria na kusababisha mauaji ya watu kadhaa. Mashirika ya habari yanaripoti takriban watu 130 wameuwawa, katika shambulizi hilo lililofanywa dhidi ya msikiti mmoja mjini Kano, mji mkubwa katika eneo la Kaskazini nchini Nigeria ambao wengi wa wakaazi wake ni Waislamu. Shambulizi hilo lilitokea hapo jana wakati wa sala ya Ijumaa. Awali kikundi cha nguvu kazi cha raia kiliundwa kulisaidia jeshi la Nigeria kukabiliana na kundi la kigaidi la Boko Haram, linalodaiwa kutekeleza shambulizi hilo. Kwa upande wake Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini amelaani mashambulizi hayo huku akisema kwa magaidi kulenga sehemu za kuabudu za waumuni wa kiislamu inaonesha kutoheshimu maisha ya binaadamu na pia kuonyesha nia yao ya kueneza ugaidi na mateso.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni