Cameron atoa heshima zake kwa wahanga wa kambi ya Auschwitz
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron leo ametoa heshima zake kwa wahanga wa mauaji ya Holocaust katika kambi ya mateso ya utawala wa Wanazi wa Ujerumani wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia ya Auschwitz, ambayo hivi sasa ni makumbusho kusini mwa Poland.
Cameron ametembelea kambi hiyo na baadaye aliangalia maonesho juu ya wahanga. Kiongozi huyo wa Uingereza alisimama kwa muda nchini Poland baada ya kuizuru Uturuki kuangalia kambi hiyo kwa mara ya kwanza.
Cameron amesema hatupaswi kuwasahau wale wote waliouwawa katika kambi hiyo na kambi nyingine, na kila mara tunapaswa kukumbuka kile kilichotokea.
Auschwitz - Birkenau imekuwa ishara ya mauaji ya halaiki ya Wanazi wa Ujerumani dhidi ya Wayahudi wa Ulaya , ambapo milioni moja wameuwawa katika kambi hiyo kuanzia mwaka 1940 hadi 1945. Kwa mujibu wa makumbusho hiyo zaidi ya watu wengine 100,000 ikiwa ni pamoja na Wapoland ambao si Wayahudi, Waroma, wafungwa wa kivita wa Kirusi na waliokuwa wakipinga utawala wa Kinazi pia wameuwawa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni