Mugabe amteua Munangagwa makamu wa rais
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amemteua waziri wa sheria Emmerson Munangagwa kuwa makamu wake mpya katika chama tawala cha ZANU-PF na serikali ya nchi hiyo leo, katika hatua ambayo imekuwa ikitarajiwa baada ya kumfuta kazi makamu wake Joice Mujuru.
Kiongozi huyo wa muda mrefu pia amemteua mwanadiploamsia wa zamani Phelekezela Mphoko kuwa makamu wa pili wa rais na kusema viongozi hao wawili wataapishwa siku ya Ijumaa.
Taarifa iliyotolewa na serikali jana imesema rais Mugabe amewafuta kazi mawaziri wake wanane kwa kuhusika na madai ya rushwa ikiwa ni pamoja na Joice Mujuru ambaye ni makamu wake wa rais.
Walioondolewa katika nyadhifa zao ni pamoja na washirika wa Joice Mujuru katika wizara za nishati, huduma za umma , na wengine sita katika idara nyingine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni