Hali bado si shwari Burundi..hii inatokana na machafuko ya kisiasa yanayoendelea baada ya Rais aliyeko madarakani Pierre Nkurunziza kutaka kuwania kwa muhula wa tatu mfululizo.
Baada ya kutofikia makubaliano ikiwemo jaribio la kutaka kumpindua lililofanywa wiki moja iliyopita kushindikana huku watu wakiendelea kaandamana kushinikiza aondoke.
Rais huyo amehairisha uchaguzi wa ubunge kwa siku kumi .
Msemaji wake Willy Nyamitwe amesema Rais huyo ameahirisha uchaguzi wa Ubunge kwa muda wa siku 10 kufuatia jaribio la mapinduzi.
Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Mei 26 na sasa utafanyika June 2 na umeahirishwa ili kupata muda wa kuwasikiliza washirika wa kimataifa pamoja na tume ya uchaguzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni