Jumatano, 20 Mei 2015

Manchester United, liverpool watoa tuzo za ubora kwa wachezaji wao!! walioshinda ni hawa


gera2
 Usiku wa jana Uongozi wa klabu ya Liverpool ulitoa zawadi kwa wachezaji wa timu hiyo ambao waliisaidia kwa kiasi kikubwa katika msimu mzima wa ligi kuu, sherehe zilifanyika katika ukumbi wa Echo Arena .
Nahodha anayeondoka Steven Gerrard ameshinda tuzo ya mafanikio ya muda mrefu ndani ya timu hiyo na anatarajia kuichezea timu hiyo kwa mara ya mwisho dhidi ya Stoke Jumapili kabla ya kuhamia LA Galaxy ya Marekani.
Mbali ya Gerrard pia Mshambuliaji kinda Raheem Sterling  ametajwa kama mchezaji bora chipukizi wa mwaka kwenye klabu hiyo licha ya baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo kumzomea kwa kitendo chake cha kytaka kuihama timu hiyo huku Philippe Coutinho akitajwa kama mchezaji bora wa mwaka.
gera
Baada ya kupokea tuzo hiyo nahodha huyo aliwashukuru makocha wake pamoja na wachezaji wenzake kwa ushirikiano waliouonyesha kwa kipindi chote  alichoichezea klabu hiyo.
mata
David de Gea na Juan Mata wakiwasili kwenye tuzo hizo
Kwa upande wa Manchester United pia walitoa tuzo kwa wachezaji wao ambapo kipa David de Gea anayetajwa kutaka kuhamia Real Madrid alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Manchester United na mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Hispania,Juan Mata ameshinda tuzo ya bao Bora la Msimu alilofunga katika mechi dhidi ya Liverpool.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni