Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk amesema umoja huo hauwezi kuwakaribisha wahamiaji wote wanaokimbilia barani Ulaya kupitia baharini na itawabidi kuanzisha sera mpya ya kuwarejesha makwao ili kukabiliana na tatizo hilo. Tusk amesema wale wanaotaka wahamiaji kuruhusiwa kuingia barani Ulaya si wa kweli, kwani haiwezekani kufungua milango yao wazi kuwahifadhi wahamiaji wote. Umoja wa Ulaya unatarajiwa hii leo kuidhinisha mpango wa kuruhusu kikosi cha jeshi la majini kupambana na wafanyabiashara haramu ya kuwasafirisha watu katika bahari ya Mediterrania baada ya boti kadhaa kuzama na kuwaua maelfu ya wahamiaji tangu mwaka huu uanze. Mawaziri wa mambo ya nje na wa ulinzi wa umoja huo wanakutana mjini Brussels hii leo na wanatarajiwa kuidhinisha mpango huo wa kutumia nguvu za kijeshi kukabiliana na tatizo la ongezeko la wahamiaji barani Ulaya.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni